Swahili New Testament Bible

Matthew 7

Matthew

Return to Index

Chapter 8

1


 

  Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata.  

 

 

-

2


 

  Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, "Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!"  

 

 

-

3


 

  Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, "Nataka! Takasika." Mara huyo mtu akapona ukoma wake.  

 

 

-

4


 

  Kisha Yesu akamwambia, "Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona."  

 

 

-

5


 

  Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, ofisa mmoja Mroma alimwendea, akamsihi  

 

 

-

6


 

  akisema, "Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana."  

 

 

-

7


 

  Yesu akamwambia, "Nitakuja kumponya."  

 

 

-

8


 

  Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.  

 

 

-

9


 

  Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, `Nenda!` naye huenda; na mwingine, `Njoo!` naye huja; na mtumishi wangu, `Fanya kitu hiki!` naye hufanya."  

 

 

-

10


 

  Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, "Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii.  

 

 

-

11


 

  Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni.  

 

 

-

12


 

  Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno."  

 

 

-

13


 

  Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, "Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini." Na mtumishi wake akapona saa ileile.  

 

 

-

14


 

  Yesu alifika nyumbani kwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, ana homa kali.  

 

 

-

15


 

  Basi, Yesu akamgusa huyo mama mkono, na homa ikamwacha; akasimama, akamtumikia.  

 

 

-

16


 

  Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.  

 

 

-

17


 

  Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: "Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu."  

 

 

-

18


 

  Yesu alipoona kundi la watu limemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake waende ng`ambo ya ziwa.  

 

 

-

19


 

  Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, "Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako."  

 

 

-

20


 

  Yesu akamjibu, "Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia."  

 

 

-

21


 

  Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu."  

 

 

-

22


 

  Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao."  

 

 

-

23


 

  Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye.  

 

 

-

24


 

  Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi.  

 

 

-

25


 

  Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe, tunaangamia!"  

 

 

-

26


 

  Yesu akawaambia, "Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?" Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.  

 

 

-

27


 

  Watu wakashangaa, wakasema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!"  

 

 

-

28


 

  Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi,*fb* ng`ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita katika njia hiyo.  

 

 

-

29


 

  Nao wakaanza kupiga kelele, "Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?"  

 

 

-

30


 

  Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa.  

 

 

-

31


 

  Basi, hao pepo wakamsihi, "Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale."  

 

 

-

32


 

  Yesu akawaambia, "Haya, nendeni." Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.  

 

 

-

33


 

  Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.  

 

 

-

34


 

  Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.  

 

 

-

Matthew 9

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: