Swahili New Testament Bible

Luke 3

Luke

Return to Index

Chapter 4

1


 

  Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.  

 

 

-

2


 

  Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.  

 

 

-

3


 

  Ndipo Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate."  

 

 

-

4


 

  Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Mtu haishi kwa mkate tu."`  

 

 

-

5


 

  Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,  

 

 

-

6


 

  "Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.  

 

 

-

7


 

  Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."  

 

 

-

8


 

  Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."`  

 

 

-

9


 

  Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu,  

 

 

-

10


 

  kwa maana imeandikwa: `Atawaamuru malaika wake wakulinde,`  

 

 

-

11


 

  na tena, `Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe."`  

 

 

-

12


 

  Lakini Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Usimjaribu Bwana Mungu wako."`  

 

 

-

13


 

  Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.  

 

 

-

14


 

  Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.  

 

 

-

15


 

  Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.  

 

 

-

16


 

  Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti.  

 

 

-

17


 

  Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:  

 

 

-

18


 

  "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,  

 

 

-

19


 

  na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."  

 

 

-

20


 

  Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.  

 

 

-

21


 

  Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo."  

 

 

-

22


 

  Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?"  

 

 

-

23


 

  Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: `Mganga jiponye mwenyewe`, na pia mtasema: `Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako."`  

 

 

-

24


 

  Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake.  

 

 

-

25


 

  Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.  

 

 

-

26


 

  Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni.  

 

 

-

27


 

  Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria."  

 

 

-

28


 

  Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana.  

 

 

-

29


 

  Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.  

 

 

-

30


 

  Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.  

 

 

-

31


 

  Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.  

 

 

-

32


 

  Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.  

 

 

-

33


 

  Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:  

 

 

-

34


 

  "We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!"  

 

 

-

35


 

  Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata kidogo.  

 

 

-

36


 

  Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!"  

 

 

-

37


 

  Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.  

 

 

-

38


 

  Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.  

 

 

-

39


 

  Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.  

 

 

-

40


 

  Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote.  

 

 

-

41


 

  Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.  

 

 

-

42


 

  Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.  

 

 

-

43


 

  Lakini yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo."  

 

 

-

44


 

  Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea.  

 

 

-

Luke 5

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: