Swahili New Testament Bible

Luke 21

Luke

Return to Index

Chapter 22

1


 

  Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.  

 

 

-

2


 

  Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.  

 

 

-

3


 

  Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.  

 

 

-

4


 

  Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa Hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao.  

 

 

-

5


 

  Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha.  

 

 

-

6


 

  Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua.  

 

 

-

7


 

  Basi, siku ya Mikate Isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa.  

 

 

-

8


 

  Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, "Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka."  

 

 

-

9


 

  Nao wakamwuliza, "Unataka tuiandae wapi?"  

 

 

-

10


 

  Akawaambia, "Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia.  

 

 

-

11


 

  Mwambieni mwenye nyumba: `Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?`  

 

 

-

12


 

  Naye atawaonyesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo."  

 

 

-

13


 

  Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.  

 

 

-

14


 

  Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.  

 

 

-

15


 

  Akawaambia, "Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.  

 

 

-

16


 

  Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu."  

 

 

-

17


 

  Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema, "Pokeeni, mgawanye ninyi kwa ninyi.  

 

 

-

18


 

  Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja."  

 

 

-

19


 

  Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, "Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka."  

 

 

-

20


 

  Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.*fd*  

 

 

-

21


 

  "Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani.  

 

 

-

22


 

  Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole wake mtu anayemsaliti."  

 

 

-

23


 

  Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya jambo hilo.  

 

 

-

24


 

  Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko wengine.  

 

 

-

25


 

  Yesu akawaambia, "Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu.  

 

 

-

26


 

  Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi.  

 

 

-

27


 

  Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.  

 

 

-

28


 

  "Ninyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu;  

 

 

-

29


 

  na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyo hivyo nami nitawakabidhi ninyi Ufalme.  

 

 

-

30


 

  Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na mtaketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.  

 

 

-

31


 

  "Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta ninyi kama mtu anavyopepeta ngano.  

 

 

-

32


 

  Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako."  

 

 

-

33


 

  Naye Petro akamjibu, "Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa."  

 

 

-

34


 

  Yesu akamjibu, "Nakwambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu."  

 

 

-

35


 

  Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, "Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?" Wakajibu, "La."  

 

 

-

36


 

  Naye akawaambia, "Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga, auze koti lake anunue mmoja.  

 

 

-

37


 

  Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: `Aliwekwa kundi moja na wahalifu,` ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake."  

 

 

-

38


 

  Nao wakasema, "Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili." Naye akasema, "Basi!"  

 

 

-

39


 

  Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata.  

 

 

-

40


 

  Alipofika huko akawaambia, "Salini, msije mkaingia katika kishawishi."  

 

 

-

41


 

  Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali:  

 

 

-

42


 

  "Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu."  

 

 

-

43


 

  Hapo, malaika kutoka mbinguni, akamtokea ili kumtia moyo.  

 

 

-

44


 

  Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.*fe* ic  

 

 

-

45


 

  Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni.  

 

 

-

46


 

  Akawaambia, "Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi."  

 

 

-

47


 

  Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.  

 

 

-

48


 

  Lakini Yesu akamwambia, "Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa kumbusu?"  

 

 

-

49


 

  Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, "Bwana, tutumie panga zetu?"  

 

 

-

50


 

  Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake la kulia.  

 

 

-

51


 

  Hapo, Yesu akasema, "Acha! Hii inatosha." Akaligusa sikio la mtu huyo akaliponya.  

 

 

-

52


 

  Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: "Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang`anyi?  

 

 

-

53


 

  Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku Hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza."  

 

 

-

54


 

  Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali.  

 

 

-

55


 

  Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja Petro akiwa miongoni mwao.  

 

 

-

56


 

  Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, "Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu."  

 

 

-

57


 

  Lakini Petro akakana akisema, "Wee! simjui mimi."  

 

 

-

58


 

  Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, "Wewe ni mmoja wao." Lakini Petro akajibu "Bwana we; si mimi!"  

 

 

-

59


 

  Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, "Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati."  

 

 

-

60


 

  Lakini Petro akasema, "Bwana wee; sijui hata unachosema!" Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.  

 

 

-

61


 

  Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: "Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."  

 

 

-

62


 

  Hapo akatoka nje, akalia sana.  

 

 

-

63


 

  Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki.  

 

 

-

64


 

  Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, "Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri tuone!"  

 

 

-

65


 

  Wakamtolea maneno mengi ya matusi.  

 

 

-

66


 

  Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.  

 

 

-

67


 

  Nao wakamwambia, "Twambie! Je, wewe ndiwe Kristo?" Lakini Yesu akawaambia, "Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki;  

 

 

-

68


 

  na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu.  

 

 

-

69


 

  Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi."  

 

 

-

70


 

  Hapo wote wakasema, "Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?" Naye akasema, "Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye."  

 

 

-

71


 

  Nao wakasema, "Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe."sw4323  

 

 

-

Luke 23

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: