Swahili New Testament Bible

John 1

John

Return to Index

Chapter 2

1


 

  Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo,  

 

 

-

2


 

  naye Yesu alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.  

 

 

-

3


 

  Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, "Hawana divai!"  

 

 

-

4


 

  Yesu akamjibu, "Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado."  

 

 

-

5


 

  Hapo mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambieni, fanyeni."  

 

 

-

6


 

  Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.  

 

 

-

7


 

  Yesu akawaambia, "Ijazeni mitungi hiyo maji." Nao wakaijaza mpaka juu.  

 

 

-

8


 

  Kisha akawaambia, "Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu."  

 

 

-

9


 

  Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi,  

 

 

-

10


 

  akamwambia, "Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!"  

 

 

-

11


 

  Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.  

 

 

-

12


 

  Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.  

 

 

-

13


 

  Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.  

 

 

-

14


 

  Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng`ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.  

 

 

-

15


 

  Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng`ombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.  

 

 

-

16


 

  Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, "Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!"  

 

 

-

17


 

  Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: "Upendo wangu kwa nyumba yako waniua."  

 

 

-

18


 

  Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, "Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?"  

 

 

-

19


 

  Yesu akawaambia, "Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu."  

 

 

-

20


 

  Hapo Wayahudi wakasema, "Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?"  

 

 

-

21


 

  Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake.  

 

 

-

22


 

  Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.  

 

 

-

23


 

  Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizozifanya.  

 

 

-

24


 

  Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote.  

 

 

-

25


 

  Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.  

 

 

-

John 3

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: