| Chapter 12 |
1 |
Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. -
|
2 |
Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu. -
|
3 |
Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja. -
|
4 |
Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake. -
|
5 |
Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. -
|
6 |
Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake. -
|
7 |
Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe. -
|
8 |
Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha. -
|
9 |
Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema. -
|
10 |
Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima. -
|
11 |
Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana. -
|
12 |
Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima. -
|
13 |
Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu. -
|
14 |
Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani. -
|
15 |
Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia. -
|
16 |
Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana. -
|
17 |
Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote. -
|
18 |
Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote. -
|
19 |
Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana." -
|
20 |
Tena, Maandiko yasema: "Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake." -
|
21 |
Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema. -
|