Swahili New Testament Bible

Hebrews 13

James

Return to Index

Chapter 1

1


 

  Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam!  

 

 

-

2


 

  Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali,  

 

 

-

3


 

  kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.  

 

 

-

4


 

  Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.  

 

 

-

5


 

  Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu.  

 

 

-

6


 

  Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na upepo.  

 

 

-

7


 

  Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote, asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa Bwana.  

 

 

-

8


 

  []  

 

 

-

9


 

  Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,  

 

 

-

10


 

  naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini.  

 

 

-

11


 

  Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake.  

 

 

-

12


 

  Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda.  

 

 

-

13


 

  Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.  

 

 

-

14


 

  Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.  

 

 

-

15


 

  Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.  

 

 

-

16


 

  Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike!  

 

 

-

17


 

  Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu.  

 

 

-

18


 

  Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake.  

 

 

-

19


 

  Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.  

 

 

-

20


 

  Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.  

 

 

-

21


 

  Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambao waweza kuziokoa nafsi zenu.  

 

 

-

22


 

  Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.  

 

 

-

23


 

  Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo.  

 

 

-

24


 

  Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.  

 

 

-

25


 

  Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.  

 

 

-

26


 

  Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.  

 

 

-

27


 

  Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.  

 

 

-

James 2

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: